Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mkoani Simiyu.
Mkoa wa Simiyu umebahatika kupata miradi mingi ya maji, hali ambayo inauweka mkoa wa Simiyu miongoni mwa mikoa mitano bora katika utoaji wa huduma ya maji nchini Tanzania.
Mradi wa kupeleka maji katika miji ya Bariadi, Itilima, Meatu na Maswa (SCRP) utakapokamilika, utapunguza kabisa adha ya upatikanaji wa maji ndani ya mkoa wa Simiyu. Sasa mkandarasi yupo katika hatua za awali za ujenzi wa matenki na ulazaji wa bomba kuanzia wilayani Busega kuelekea kwenye mji wa Bariadi.

Waandishi wa habari kutoka CLOUD MEDIA wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa BUSEWASA katika uzinduzi wa kampeni ya Raisi kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji iko mwa mwa mwa mkoani Simiyu. Oct 11, 2024
BUSEWASA yatoa ofa ya kurejesha maji bila gharama kwa wateja waliositishiwa huduma ya maji ndani ya wiki ya huduma kwa wateja.
Kitengo cha huduma kwa wateja wameitumia vyema wiki ya huduma kwa wateja kwa kutoa ofa ya kurejeshewa maji bure kwa wateja waliositishiwa maji kwa kutolipa bili zao.
Wateja hao wanatakiwa kulipia bili zao tu ili warejeshewe maji ndani ya wiki ya huduma kwa wateja.
Ofa hii itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa kumi, hivyo wateja wote waliositishiwa maji kwa sababu ya bili walipe madeni yao na warejeshewe maji bila gharama.

BUSEWASA waadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kutoa ofa ya marejesho ya maji bure kwa wateja waliositishiwa. Oct 11, 2024
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Faiza Salim amewaongoza wajumbe Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na kamati ya Siasa wilaya ya Busega kutembelea na kuona maendeleo ya mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi Mkoani Simiyu tarehe 20 Mei, 2025.
Ambapo alipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo iliyowasilishwa na Eng.Paul Hezron,kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Busega(BUSEWASA) na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Mhe mkuu wa wilaya alimtaka mkandarasi kujitahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi ili kuweza kukamisha mradi huo kwa wakati kulingana na mkataba unavosema.
Aidha alilisisitiza kuwa upatikanaji wa ajira katika mradi wapewe kipaumbele wakazi wanao zungukwa na mradi huo.
Mhe mkuu wa wilaya pia alitoa rahi kwa wananchi waliolipwa fidia tayari ya maeneo ambayo yatajengwa miundombinu ya mradi huo kupisha haraka ili kuruhusu utekelezaji wa mradi kuendelea.
Pia Mhe.mkuu wa wilaya alimshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani kutoa fedha zaidi ya Bilioni 440 kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo ili kuweza kuwatua ndoo kichwani kinamama wa Mkoani Simiyu ikiwemo wananchi wa wilaya ya Busega.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Faiza Salim, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Siasa wilaya ya Busega wakitembelea mradi wa kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi - SCRP 20/05/2025 May 24, 2025