Historia
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Busega ni mamlaka ya maji ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya maji na usafi wa mazingira na 5 ya mwaka 2019 na kupewa GN namba 216 ambayo ilitangazwa katika gazeti la serikali tarehe 26/2/2021. Maeneo ya huduma katika GN ni Lamadi, Mkula na Nyashimo.
Katika maeneo yote ya huduma. Mamlaka ya maji kupitia mradi wa maji Lamadi, tunatoa huduma ya majitaka ambapo kuna mabwawa ya kutupia maji taka yenye uwezo wa kutoa huduma kwa wastani wa kaya 5,760 kwa mwaka.
Maeneo yanayopata huduma ya maji kwa sasa ni Lamadi, Kabita, Nyashimo, Mkula, Lutubiga, Mwamanyili na Kiloleli.