Maunganisho Mapya

 Imewekwa: 08 October, 2024

Maunganisho Mapya


UTARATIBU WA MAUNGANISHO MAPYA

 1. Fomu ya maombi

  • Mteja anapaswa kujaza fomu ya maombi ambayo inapatikana bure kwenye ofisi zote za BUSEWASA na kwenye tovuti ya BUSEWASA. Unaweza kupakua HAPA

2. Viambatisho vinavyohitajika  

  • Picha moja (Passport Size)
  • Nakala ya kitambulisho (Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga kura, Leseni ya udereva ama kitambulisho kingine kinachotambulika na serikali)
  • Kwa taasisi/mashirika watapaswa kupiga muhuri sehemu ya picha na kuweka viambatisho vya usajili wa taasisi/mashirika yao.

3. Upimaji (Survey) 

  • BUSEWASA itafanya upimaji kwa mteja aliyekamilisha kujaza fomu ya maombi na viambatisho vinavyohitajika na kuiwasilisha ofisi za BUSEWASA ndani ya siku saba za kazi.

4. Makadirio ya Gharama  

  • BUSEWASA itaandaa gharama zote za makadirio zinazohitajika kwa ajili ya maunganisho mapya.
  • Ununuzi wa vifaa vipya vya kuunganisha huduma ya maji itafanywa na BUSEWASA kwa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma.

5. Taarifa kwa mteja. 

  • Baada ya makadirio ya gharama, BUSEWASA itamjulisha mwombaji kupitia ujumbe mfupi (SMS) jumla ya gharama ya maunganisho. Gharama hizi pia zitapatikana kwa mteja kufika ofisi za BUSEWASA kupata nakala ya (BOQ) ikiwa na mtililiko wa vifaa na gharama zake kwa atakayehitaji.

6. Malipo 

  • Makadirio ya gharama yatalipwa na mteja kupitia namba ya malipo ya serikali – Control Number,  aliyopokea kwenye SMS au kwenye BOQ.

7. Utekelezaji wa maunganisho mapya.

  • Baada ya mteja kukamilisha malipo ya gharama za maunganisho mapya BUSEWASA itamfanyia mteja maunganisho ya huduma ya majisafi.
  • Baada ya maunganisho kukamilika BUSEWASA itafanya majaribio ya kuhakiki ufanisi wa maunganisho.
  • Dira ya maji itafungwa kwa mteja bure.